Wizara_afyatz's Instagram Audience Analytics and Demographics

@wizara_afyatz

Tanzania

Ukurasa rasmi wa Wizara ya Afya Tanzania 🇹🇿 S.L.P 743 Dodoma Barua pepe;
mawâ–“â–“â–“â–“â–“@afya.go.tz
Tanzania

Business Category

Government Agencies

Get Our Influencer Rate Card Today!

A brand new way for you to compare the rates of influencers across the world.

Learn More

PROFILE OVERVIEW OF WIZARA_AFYATZ

Average engagement rate on the posts is around 0.03%. The average number of likes per post is 129 and the average number of comments is 5.

Wizara_afyatz loves posting about Product Education, Politics.

Check wizara_afyatz's audience demography. This analytics report shows wizara_afyatz's audience demographic percentage for key statistic like number of followers, average engagement rate, topic of interests, top-5 countries, core gender and so forth.

Followers
415,576
Avg Likes
129
Avg Comments
5
Posts
5,102

GENDER OF ENGAGERS FOR WIZARA_AFYATZ

Female
0 %
Male
0 %

MENTIONED HASHTAGS OF WIZARA_AFYATZ

RECENT POSTS

28 0

Siku ya Usalama wa Chakula Duniani. Chakula salama afya bora #jiandaekuhesabiwasensa2022 2022 @tmda_tanzania

41 3

Huduma za Wizara ya Afya hutegemea idadi ya watu, tujitokeze kuhesabiwa tarehe 23/08/2022 Jali Afya Yako… Jiandae kuhesabiwa 🇹🇿

170 6

Paris, Ufaransa Waziri wa Afya Ummy,leo tarehe 6 Juni, 2022 amewasili katika Jiji la Paris , Ufaransa kuhudhuria kikao cha Jumuia ya Wafadhili wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto (Global Financing Facility - GFF). Akiwa nchini Ufaransa Waziri Ummy amekutana na Mawaziri wenzake kutoka Sierra Leone, Bukinafaso, Niger na nchini nyingine kwenye kikao cha kuzungumzia changamoto zinazokwamisha katika utoaji huduma bora. Akizungumza kwenye kikao hicho Waziri Ummy amesema upungufu wa watoa huduma wenye ujuzi ni changamoto kubwa inayoikabili Tanzania katika kuhakikisha inatoa huduma bora. Aidha, ubora wa mafunzo yanayotolewa na kile wanachokipata wahitimu ametaja kuwa ni tatizo linalochangia kwenye matokeo yasiyotarajiwa kwenye vituo vya kutolea huduma. Ameongeza kuwa Tanzania ina shida kwenye kutumia watoa huduma ngazi ya jamii wakati uzalishaji wa watoa huduma wenye ujuzi likiwa kubwa. Swali linagonga vichwa ni je "tumchukue asie na ujuzi au mwenye ujuzi" ili kuweza kupata matokeo yenye tija zaidi

201 2

Cairo , Misri Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Madaktari Mabingwa kutoka Tanzania ambao wanasoma katika Chuo Kikuu cha Alexandria, Misri leo tarehe 6 Juni, 2022 Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania Misri , Dr Emmanuel Nchimbi na Mfamasia Mkuu wa Serikali Ndg . Daudi Msasi. Katika kikao hicho Prof. Makubi ameahidi kufanyia kazi changamoto za Madaktari hao ambao wapo mafunzoni ikiwa ni pamoja na kuongeza udhamini na kupata mafunzo zaidi ya vitendo wakiwa nyumbani Tanzania.

176 5

Cairo,Misri Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof.Abel Makubi ameshiriki Mkutano wa nne wa Mawaziri wanaohusika na Afya, Lishe ,idadi ya watu na udhibiti wa dawa za kulevya Barani afrika unaofanyika Cairo,Misri.Prof. Makubi amehudhuria Mkutano huo wa Nne akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu. Mkutano huo umejadili ushiriki wa nchi wanachama wa umoja wa Afrika katika kuimarisha Huduma za Lishe, mapambano dhidi ya dawa za Kulevya pamoja na kuimarisha Taasisi ya Afrika ya kudhibiti magonjwa (Afrika CDC). Aidha, Prof. Makubi pia ameshiriki ufunguzi wa maonesho ya Afya mjini Cairo, ufunguzi huo umefanywa na Rasi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe, Abdel Fattah El-Sisi na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Zimbabwe na Mawaziri mbalimbali kutoka Afrika. Katika Mkutano huo Tanzania imechaguliwa kama Makamu Mwenyekiti wa Kwanza.

127 10

WAZIRI UMMY ATAKA CHANJO YA MALARIA IANZE KUTOLEWA NCHINI Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameitaka Bodi ya Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na kamati ya chanjo ya taifa kuharakisha mchakato wa kufanya tathmini ya chanjo ya Malaria ili Serikali ianze kutoa kwa wananchi. Waziri Ummy amesema hayo leo katika uzinduzi wa Baraza jipya la Taasisi hiyo uliofanyika leo hii Jijini Dar es salaam. Waziri Ummy amesema NIMR imeshiriki kufanya utafiti wa kupata chanjo ya malaria ambayo tayari imesha thibitishwa na shirika la afya Duniani kuwa inafaa kutumika. "Kwahiyo naomba mfanye mchakato haraka wa kuithibitisha chanjo, kwa kuanzia chanjo hiyo itatolewa kwa yule ambae yupo tayari kulipia kwa gharama zitakazo wekwa lakini Serikali itaangalia kama itaweza kutoa kwa watoto chini ya miaka mitano". Amesema Waziri Ummy. Aidha, Waziri Ummy ameitaka NIMR kuweka nguvu katika kuhakikisha wanafanya tafiti zenye kuleta manufaa kwa wananchi ili kuiwezesha Serikali kuchukua maamuzi haraka katika utoaji wa huduma za Afya Nchini. "Zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanatumia dawa za tiba asili lakini watu wanakunywa dawa bila kufuata dozi maalum, sasa naitaka NIMR itupe ushahidi wa kisayansi juu ya dawa hizo na dozi inayo hitajika kwa dawa husika". Ameongeza Waziri. Nae Mganga mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe amelitaka Baraza hilo kuwa kiunganishi kizuri kati ya sekta ya Afya na watafiti mbalimbali wa masuala ya Afya wa ndani na nje ya nchi. "Natumaini Bodi itasaidia kuweka mazingira bora katika kuifahamisha Wizara kwa ajili ya maamuzi na utungaji wa sera lengo ni kuharakisha mchakato wa kupata vibali bila kuathiri thamani na ubora wa tafiti". Amesema Dkt. Sichalwe Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Andrew Kitua wakati wa kutoa shukurani ameahidi kushirikiana na wizara pamoja na taasisi zingine za utafiti ili kufanya tafiti zenye kuleta manufaa kwa wananchi. MWISHO.

243 0

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ndung’unyi, iliyopo katika kata ya Ndung’unyi Halmashauri ya Ikungi, Mkoa wa Singida, Dkt. Advera Thadeo amesema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kiasi cha shilingi Milioni 20 kupitia mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa vyoo vitatu ikiwemo choo cha walemavu, kuweka mfumo wa maji safi katika sehemu zote za kutolea huduma pamoja na sehemu za kunawia mikono. “Mpaka sasa utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 97 na mafundi wanaendelea na kazi kukamilisha asilimia tatu zilizobaki ili mradi ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kama yalivyo matarajio ya mradi wenyewe”, ameeleza Dkt. Advera Dkt. Advera ameongeza kuwa mradi huo ukikamilika utakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa kata ya Ndung’unyi pamoja na watumishi wa zahanati hiyo kwani changamoto itakua imetatuliwa na kuleta ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi. @ummymwalimu @maelezo @msamajiwaserikali @ortamisemi #AfyaKwanza #JaliAfyaYako

56 0

FEDHA ZA MIRADI ZIENDANE NA THAMANI YA MRADI- MWAKITALIMA Na. WAF, IKUNGI - SINGIDA Mratibu wa Mradi wa Huduma Endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, kutoka Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima ameitaka mikoa 17 na Halmashauri 86 nchini zinazotekeleza mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (Sustainable Rural Water Supply and Sanitation) kuhakikisha kazi zinazotekelezwa chini ya mradi huo zinakua na thamani inayo akisi fedha iliyotolewa yaani “Value for Money”. Mwakitalima ametoa kauli hiyo leo wakati akiendelea na zoezi la usimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mkoani Singida ambapo amesema fedha iliyotolewa iwe na uwiano sawa na kazi iliyofanyika ili kuongeza tija ya mradi huo kwa wananchi wa eneo husika. @ummymwalimu #jaliafyayako #AfyaKwanza

116 2

FEDHA ZA MIRADI ZIENDANE NA THAMANI YA MRADI- MWAKITALIMA Na. WAF, IKUNGI - SINGIDA Mratibu wa Mradi wa Huduma Endelevu wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, kutoka Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima ameitaka mikoa 17 na Halmashauri 86 nchini zinazotekeleza mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (Sustainable Rural Water Supply and Sanitation) kuhakikisha kazi zinazotekelezwa chini ya mradi huo zinakua na thamani inayo akisi fedha iliyotolewa yaani “Value for Money”. Mwakitalima ametoa kauli hiyo leo wakati akiendelea na zoezi la usimamizi wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini, katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mkoani Singida ambapo amesema fedha iliyotolewa iwe na uwiano sawa na kazi iliyofanyika ili kuongeza tija ya mradi huo kwa wananchi wa eneo husika. “Nasisitiza kwa ujumla Halmashauri zote zinazotekeleza mradi huu kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi kwani inaonekana wako nyuma na sisi tunataka mradi ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi”. Amesisitiza Mwakitalima. Vile vile Mwakitalima ameongeza kuwa halmashauri hizo zinatakiwa kuhakikisha kunafanyika usimamizi wa karibu ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mradi. Pia Mwakitalima amekumbushia baadhi ya shughuli zilizokuwa zimesaulika nazo ziweze kufanyiwa kazi ili kuleta ukamilifu wa mradi na kwa manufaa makubwa yaliyokusudiwa. Aidha, Mwakitalima amemtaka Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Puma iliyopo katika kata ya Puma Halmashauri ya Ikungi kuhakikisha ifikapo Jumanne ya wiki ijayo vyoo vilivyojengwa chini ya mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini mwaka jana vinaanza kutumiwa na wananchi wanaofata huduma katika zahati hiyo. “Haiwezekani vyoo vimekamilika tangu mwaka jana na mfumo wa maji upo vizuri halafu havitumiki eti mnasubiri vizinduliwe, hakuna kitu kama hicho vyoo vitoe huduma kwa wananchi ili kuleta manufaa yaliolengwa katika mradi”. Ameeleza Mwakitalima. Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ndung’unyi, iliyopo katika kata ya Ndung’unyi Halmashauri ya Ikungi, Mkoa wa Singida, Dkt. Advera Thadeo amesema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia .

97 2

Ruvuma ivume kwa maendeleo Hongereni sana Ruvuma #AfyaKwanza #JaliAfyaYako

53 2

Waziri Ummy akiri kuwepo kwa changamoto ya utoaji wa huduma katika taasisi ya mifupa ya MOI. Aagiza utaratibu uwekwe wa kuwahudumia wagonjwa bila kero huku akiahidi ujenzi wa jengo jipya litakalosaidia kuondoa msongamano.

643 13

Waziri @ummymwalimu amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface kufuatilia na kukomesha tabia ya baadhi ya madaktari kuwaandikia wagonjwa vipimo na kuwataka kwenda kufanya katika Hospitali binafsi japokua vipimo hivyo vinapatikana hapo.

* Copyright: Content creators are the default copyright owners. These Images are published on public domains and respective social media for public viewing.

PEOPLE ALSO VIEWED

3.8K
-
1.95 %
Tanzania Shopping
35.9K
-
0.30 %
Tanzania Entertainment and Music, News, Singer
24.7K
-
1.40 %
Tanzania Entertainment and Music
1.2K
-
-
Tanzania Education, Upskilling
33.6K
-
-
Tanzania Product Education, Auto and Vehicles, Home and Garden, Soccer
1.7K
15 / post
0.96 %
Tanzania Finance, Celebrities, Cars & Motorcycles, Design
73.7K
-
0.03 %
Tanzania Fashion and Accessories, Beauty and Self Care, Music
72.2K
-
0.05 %
Tanzania Food, Health and Medical Services, Music, Singer
4.1K
-
0.53 %
Tanzania Entertainment and Music
6.3K
-
16.16 %
Tanzania Entertainment and Music, Music
104.8K
-
1.21 %
Tanzania Education, Singer
19.7K
-
0.05 %
Tanzania Beauty and Self Care, Health and Medical Services, Singer, Spa Beauty Personal Care, Beauty, Cosmetic & Personal Care, Lifestyle Services
34.7K
363 / post
1.82 %
Tanzania Fashion and Accessories, Romance and Wedding, Family, Singer, Celebrities, Film, Music & Books, Animals & Pets, Humor
5.8K
-
0.71 %
Tanzania Entertainment and Music
6K
-
0.96 %
Tanzania Entertainment and Music